NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara


Manyara Regional Referral Hospital, through the Ministry of Health, is advertising volunteer positions for the following cadres:-

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, kupitia Wizara ya Afya inatangaza nafasi za kujitolea kwa kada zifuatazo:-

Recommended:


AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II NAFASI (6)

SIFA ZA MWOMBAJI:-

  • a)Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • b)Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania(TNMC)

KAZI ZA KUFANYA

  • Kutoa huduma za uuguzi.
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake Kuelimisha wagonjwa na jamii.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

MHUDUMU WA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI NAFASI (2)

SIFA ZA MWOMBAJI:
Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na amepata mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya afya, ngazi ya afya ya jamii katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na amepata cheti cha NACTE.

KAZI ZA KUFANYA

  • Kupokea na kuhifadhi miili kutoka ndani na nje ya hospitali Kuweka taarifa sahihi za miili iliyohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
  • Kuhakikisha kuwa miili inahifadhiwa katika viwango sahihi, kuzingatia dawa na kutenga “infectious” na “non infectious”
  • Kufanya usafi wa vifaa vya kazi, usafi wa mazingira Kufanya shughuli nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi.

MSAIDIZI WA HESABU DARAJA II NAFASI (3)

SIFA ZA MWOMBAJI:
Mwombaji awe na Stashahada katika fani ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au cheti cha ATEC II kinachotolewa na NBAA.

KAZI ZA KUFANYA

  • Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
  • Kutunza Kumbu kumbu za hesabu.
  • Kupeleka nyaraka za uhasibu benki.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Read Also:

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAOMBAJI WOTE

  • Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania.
  • Mwombaji awe na cheti cha ufaulu kidato cha nne.
  • Barua zote za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya kuhitimu elimu, taaluma, cheti cha kuzaliwa na picha za rangi mbili za hivi karibuni (passport size).
  • Mwombaji aambatanishe maelezo binafsi (CV).
  • Mwombaji awe na ujuzi wa kutumia kompyuta (MS Excel & MS Word).
  • Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45 “Testimonials result slips” HAIZITAKUBALIWA.
  • Mwombaji awe mwenye tabia na nidhamu nzuri,hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani au kufungwa
    za vyeti zithibitishwe kwa kugongwa mhuri mwanasheria/hakimu
    (Uzoefu katika taaluma/kada husika atapewa kipaumbele).

Mwombaji atume maombi kwa njia ya posta au kuwasilisha Ofisi ya Mganga Mfawidhi kabla ya tarehe 13.01.2026. saa 9:30 Alasiri katika anuani ifuatayo:-
MGANGA MFAWIDHI,
HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA,
S.L.P. 577,
MANYARA.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Expresstz Jobs Centre