AJIRA ZA WALIMU KUJITOLEA SERIKALINI

ads1



Sifa na Vigezo kwa Walimu wa Kujitolea 2025

Serikali kupitia wizara ya TAMISEMI Wameruhusu Halmashauri mbalimbali kuajiri waalimu kwa kujitolea lakini kwa malipo maalumu. 

Mwalimu wa kujitolea katika Shule za Elimu ya awali, Msingi, Sekondari, na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi anahitajika kuwa na sifa zifuatazo; 

✓Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18. 

✓Awe Mhitimu aliyefaulu mafunzo ya Ualimu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. 

✓Awe Mmiliki wa vyeti halisi vya kitaaluma na kitaalam. 

✓Awe na Wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Umma au viongozi wa Serikali za Mitaa/Kata au Viongozi wa dini. 

✓Awe hajawahi kuhukumiwa kwa makosa ya kijinai au kuwa na kesi ya jinai. 

✓Awe na tabia na mienendo inayokubalika na jamii. Utaratibu wa Kupata Walimu wa Kujitolea ni kama ifuatavyo:

 ✓Kamati za shule/Vyuo kubainisha mahitaji halisi ya walimu. 

✓Kipaumbele kitolewe kwa Waombaji waliojishughulisha na Shule/Chuo husika awali. 

Waombaji kutoka maeneo yanayozunguka Shule/Chuo.
Kuweka matangazo kwenye
Mbao za matangazo za Halmashauri, Kata, Shule, na Vyuo.
✓Vyombo vya habari kama Redio, Mitandao ya Kijamii, na Runinga.
✓Waombaji kuwasilisha Maombi kwa, Mkurugenzi wa Halmashauri au Mkuu wa Chuo, ikiwa na anuani kamili na mawasiliano (namba za simu/barua pepe).


✓Uchambuzi wa Maombi, Kamati za Shule/Vyuo kushiriki kikamilifu kuchambua maombi.


✓Orodha ya walimu waliochaguliwa kutangazwa kwenye mbao za matangazo na vyombo vya habari.


Walimu waliochaguliwa kujulishwa kwa barua.


✓Barua za Uteuzi zinaweza kufutwa kabla ya kusaini Mikataba ikiwa Serikali itaona ni lazima.ads2