Majina ya walioitwa kwenye mafunzo zimamoto

Tags

ads1

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wahusika wote wanatakiwa kufika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopoChogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 18  Mei, 2025 bila kukosa; kwa ambaye hatafika chuoni kwa tarehe zilizopangwa hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Recommended:


Kufika chuoni shuka kituo cha Kabuku kilichopo kilometa 12 toka chuoni. Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea kwa tarehe zilizotajwa hapo juu, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.

Mhusika atapaswa kujigharamia nauli ya kwenda sambamba na chakula na malazi kwa siku zote ambazo atakuwa hajapokelewa Chuoni. Mhusika anapaswa kuja akiwa na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioombea pamoja na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba na leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva.

Read Also:

Vyeti vyote tajwa hapo juu viwe na nakala tatu kwa kila cheti pia vyeti hivyo vitakaguliwa na kwa ambaye majina yake yatatofautiana kati ya vyeti vya shule/taaluma, NIDA na cheti cha kuzaliwa watarudishwa na nafasi zao zitachukuliwa na wengine.

DOWNLOAD PDF FILE HAPA

ads2

This Is The Newest Post