Majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi

ads1




ANGAZO LA KURIPOTI SHULE YA POLISI MOSHI KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA

Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo. Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
 
 

Recommended:

1. Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.
 
2. Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
 
3. Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.

Read Also:

 
4. Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari.
 
5. Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo: i) Traki suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, bukta mbili (2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya bluu.

PAKUA HAPA PDF FILE YA MAJINA 

ads2