
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne wenye sifa zifuatazo: –
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I-
- Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.
Recommended:
- Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
- Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8″) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4″) kwa wanawake.
- Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
- Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.
- Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
- Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
- Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
- Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
- Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili.
Read Also:
Nafasi za kazi Jeshi laPolisi March 2025
FANI ZINAZOTAKIWA KWA KILA NGAZI YA ELIMU TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.